Muendelezo wa mazoezi kwa mama mjamzito.
Kama ulikuwa unafanya
mazoezi kabla ya ujauzito unaweza kuendelea na mazoezi yafuatayo.
Kuogelea:
Uzuri
wa zoezi hili ni kwamba halihitaji nguvu nyingi linasaidia kurelax na misuli yote ya mwili
inafanya kazi. Unaweza kuogelea kwa dakika 20 hadi 35 lakini uchukue break pale
utakapoona umechoka au kuishiwa na nguvu au pumzi. Kuogelea pia kunasaidia
kupunguza maumivu yatokanayo na miguu kuvimba.
Kutembea: Ni zoezi zuri sana kwa mwanamke mjamzito. Zoezi
hili linaweza kufanywa dakika 20 had 35 kwa siku. Zoezi hili linapunguza
stress, linasaidia chakula kushuka vizuri na digestion. Pia linasaidia katika
kuweka sawa uti wa mgongo. Tatizo la uti wa mgongo kutokunyooka linasababishwa
na tumbo kuongezeka na kukosekana kwa balance kwenye mwili. Hiki ni chanzo cha
maumivu ya mgongo. Kumbuka kuchuka break na kupumzika pale utakaposikia uchovu.
Kucheza Muziki: Mama mja mzito anaweza
kucheza mziki kama zoezi hasa hasa mziki wa belly dancing wa kunyonga kiuno na
miziki aina ya salsa. Hii inasaidia katika kulainisha misuli ya uzazi tayari
kwa kujifungua, kusaidia kujifungua kwa urahisi na kupona kwa haraka zaidi
baada ya kujifungua, kupunguza michirizi ya tumbo(stretch marks) inayojitokeza
kwa ajili ya ngozi ya tumbo kuvutwa, pia inasaidia confidence ya mwanamke
kujiona bado ana mvuto, kuondoa stress, kusaidia na balance, kupunguza
maumivu ya mgongo na kusaidia kunyoosha uti wa mgongo.
Pia unaweza kuendesha baiskeli ila uangalie balance
usianguke na usiendeshe sehemu zenye msongamano wa watu au traffic ikiwezekana
tumia baiskeli special za mazoezi ndani ya gym (stationary bikes).
Mazoezi mengine ni yale
yanayofundishwa ndani ya gym na mwalimu spesho kama yoga au pilates.Yoga
inasaidia kurelax kama tulivyoongelea post iliyopita umuhimu wa kurelax. Yoga
husaidia mzunguko wa damu na kupunguza matatizo ya uvimbe hasa hasa kwenye
miguu,kupunguza stress kusaidia na usingizi, kuondoa kemikali na taka ndani ya
mwili, kusaidia kupumua vizuri, kunyoosha misuli ya uzazi na ya tumbo ili
kusaidia kupunguza maumivu wakati wa kujifungua, kupunguza maumivu ya mgongo,
kusaidia na kichefu chefu na kupunguza anxiety na mood swings.
Haya ni baadhi tu ya
mazoezi ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kufanya katika kipindi hicho
ikiwa afya yake inaruhusu. Mazoezi haya hayafanywi yote kwa wakati mmoja. Bali
unaweza kuchagua yale unayopenda kufanya na kuweka ratiba ili usichoke. Kama
Jumatatu unafanya kuogelea, Jumanne kutembea, Jumatano Yoga, Alhamisi Kucheza
mziki n.k Kufuatana na vile unavyopenda na kujisikia. Katika post zijazo
tutaongelea mazoezi maalumu yanayotakiwa kufanywa na wamama wajawazito katika
kujitayarisha na kujiweka sawa na suala zima la kujifungua.
No comments:
Post a Comment