UMUHIMU WA MAZOEZI KWA MWANAMKE MJAMZITO:
Sehemu Ya Kwanza - Relaxation
Kuzaa ni tukio linalohusisha viungo
na misuli mbali mbali katika mwili wa mwanamke. Katika kujitayarisha kwa tukio
hili ni vizuri kuendelea na mazoezi mbali mbali ili kuwa fit kwa ajili ya hili
tukio na kuzuia complications hapo baadaye. Mazoezi muhimu hasa hasa ni
yale maalumu kwa mwanamke mjamzito. Haya Mazoezi yatasaidia kuwa na stamina wakati
wa labour na kujifungua.
KUMBUKA:
·
Wakati unafanya mazoezi hakikisha kuwa husikii
maumivi yoyote na ukipatwa na maumivu hakikisha unaonana na daktari haraka
iwezekanavyo. Kumbuka usilalie mgongo wakati wa kufanya mazoezi au usifanye
mazoezi aina ya jogging (kukimbia) au kuruka ruka (bouncing) na hakikisha
mdundo wa moyo (pulse) na temperature yako ya mwili ziko sawa. Kunwya maji
mengi kuzuia dehydration na angalia balance yako kama iko sawa ili kuzuia
kuanguka.
Katika kipengele hiki cha kwanza
tutaongelea umuhimu wa mazoezi aina ya Relaxation kwa mama mjamzito. Je ulijua
ya kwamba mwili usiporelax katika labor hormone aina ya epinephrine inatolewa? Hii hormone inazuia process asilia ya labor
au inaweza kuleta complications katika labor. Kujifunza kurelax wakati wa
ujauzito kutasaidia sana kupunguza maumivu wakati wa labor kwa sababu mwili na
misuli inapokakamaa ndio maumivu yanapozidi. Ila ukijifunza kutune mwili wako
kulegea na kurelax utaweza kupungza maumivu naturally kwa kiasi kikubwa. Na ili
kumaster hii tekniki na kuweza kurelax wakati wa labour unabidi upractice siku
zote za ujauzito wako.
Aina tatu za relaxation:
1) relaxation ya mwili - yaani kulegeza misuli yote ya mwili
wako ili kuondoa maumivu na tension. Wakati wa labor uterus ina contract na
kwenda mbele kuhakikisha mtoto anashuka chini. Kama mama atakuwa yuko stressed
au tensed katika kipindi hiki basi lazima atasikia maumivu makali.
Mume au mtu wa karibu kwa mwanamke
anabidi ampapase kwenye sehemu mbali mbali ya mwili wake kama mabega, mikono,
hips, mapaja ,magoti , miguu , kichwani nywele ili kumsaidia kurelax na
kutulia. Pia kumpa massage katika maeneo haya au kuweka pressure kwenye sehemu
zenye maumivu kwa kutumia taulo lenye maji au chupa yenye maji ya baridi au
vuguvugu kiasi kama sehemu za mgongo na shingo. Iwapo utafanya hili zoezi na
muemeo kila siku basi ataweza kujua jinsi mwili wako ulivyo ukikakamaa na
kuconcentrate kupapasa sehemu hii ili kukutuliza.
Mfano wa zoezi: mume atamwambia mke
akaze misuli ya mikono, akishaikaza mume atashika misuli ya mikono kwa
kuipapasa na kuimassage mpaka misuli ireleax endelea hivi na viungo na maeneo
mengine ya mwili wa mwanamke.Mwanaume anabidi amuulize mke wake anapenda kushikwa
au kupapaswa vipi ili kusaidia kurelax zaidi. Pia mwanamke ataweza
kutambua tofauti kati ya mwili wake ukiwa relaxed au stressed. Hii itamsaidia
kujua jinsi ya kurelax viungo vyake wakati wa labor akisikia maumivu. Katika
hili zoezi mnaweza kutumia mafuta ya aina mbali mbali pia
2) relaxation ya akili - Kuhakikisha mawazo yako ni mazuri yaani hamna
mawazo negative hii inawezekana kwa kusikiliza muziki murua utakaosaidia
kurelax au kusoma hadithi nzuri, mume anaweza akamwandikia mkewe insha nzuri za
kumpa moyo na kumuonyesha anamjali na umuhimu wake katika kipindi hiki, kama ni
watu wadini kusali na kuwepo karibu na Mungu kwa kusoma vitabu vya dini.
Mwanamke akiwa na msongomano wa mawazo anaweza akasikia stress ambayo itaongeza
maumivu kwenye mwili. Ni vizuri kufikiria vitu vizuri vya kufurahisha na
kutuliza mawazo. Mume anaweza kumkumbusha mke wake vitu vizuri vilivyowahi
kutokea au anaweza akamsifia kwa kumwambia anafanya vizuri na umebaki mda
kidogo tu hadi mtoto afike n.k
Mfano wa zoezi: Baada ya zoezi la kwanza la kummmasage mwanamke, mwili
wake ukisha relax vya kutosha basi mme anaweza akamwekea mziki mzuri, akamsomea
insha yaani poem/hadithi/ kitabu cha dini / kusali au kumwambia maneno mazuri
ya kumuencourage huku akiendelea kumassage katika kipindi hiki mwanamke anaweza
kufumba macho ili kurelax zaidi. Hii inasaidia pia muda kupita na
muda unavyozidi kupita basi labor stage inaendelea kusonga mbele bila mke
kujitambua.
3) relaxation ya emotions/hisia - kuhakikisha roho inajisikia
nyeupe. Hapa mume au mtu aliye karibu na mwanamke anabidi awe karibu naye ili
kuhakisha anaondoa mashaka yoyote kwa mwanamke. Kwa kumpa maneno mazuri ya
kumsupport na kumpa faraja. Pia kumsikiliza kama kuna chochote angependa
kuongelea na kumfariji. Kumuuliza anategemea nini kutoka kwake vitu gani
angependa vifanyike na kuhakikisha vinatekelezwa. Hii itamsaidia mwanamke kuwa
comfortable kuondoa uoga na labour kuendelea vizuri. Hasa hasa kuondoa uoga.
Hapa umuhimu wa mwanaumme ni kumfanya mwanamke asikie kama analindwa, anapendwa
na anaweza kumtegemea mwenzi wake katika kipindi hiki.
Haya mazoezi yanatakiwa kufanywa
dakika 20 mara mbili kwa siku, kila siku ya ujauzito. Ukianza unaweza anza
dakika 10 kwa siku halafu ongeza mpaka dakika 15 kwa siku na kuongeza
kidogo kidogo mpaka mfikie dakika 20. Mara moja mama anaweza akafanya akiwa
peke yake na mara ya pili akiwa na mtu wa karibu atakayekuepo wakati wa
kujifungua ikiwa ni mume, ndugu au rafiki wa karibu.
UMUHIMU WA MAZOEZI KWA MWANAMKE MJAMZITO
Sehemu Ya Pili - Mazoezi ya kawaida
Jana tuliongelea mazoezi ya
relaxation na umuhimu wa mazoezi haya kwa mama mjamzito hasa hasa kumtuliza na
kuzuia misuli kukaza wakati wa kujifungua kitu ambacho kitaongeza uchungu wa
labour. Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza
kuendelea kuyafanya kila siku ya ujauzito wake na umuhimu wake. Mazoezi
yanasaidia:
- Kupata usingizi mzuri usiku.
- Kuondoa stress
- Kulegeza na kunyoosha misuli ya uzazi na kuitayarisha kwa kazi ya kujifungua
- kupunguza kichefu chefu(morning sickness) na kiungulia(heartburn)
KUMBUKA:
Wakati
unafanya mazoezi hakikisha kuwa husikii maumivi yoyote na ukipatwa na maumivu
hakikisha unaonana na daktari haraka iwezekanavyo. Kumbuka usilalie mgongo
wakati wa kufanya mazoezi au usifanye mazoezi aina ya jogging (kukimbia) au
kuruka ruka (bouncing) na hakikisha mdundo wa moyo (pulse) na temperature yako
ya mwili ziko sawa. Kunwya maji mengi kuzuia dehydration na angalia balance
yako iko sawa ili kuzuia kuanguka.
Asante sana nmejifunza kitu
ReplyDeleteDah km wakukufanya stress zitoke ndio msababishaji je utafanyaje ili roho iwe nyeupe
ReplyDelete