AINA ZA MADINI YANAYOFAA KWA MAMA MJAMZITO
Aina ya vitamini C na madini
ya chuma yaweza kupatikana katika maini, maharagwe, mboga zenye majani mabichi,
njugu, na nafaka zilizoongezwa vitamini na madini mbalimbali. Kuchanganya
chakula chenye vitamini ya C, kama matunda yaliyotoka shambani karibuni,
pamoja na chakula chenye madini ya chuma huongeza madini hayo mwilini.
Ongezeko linalopendekezwa kwa mwanamke mwenye uzito unaofaa
anapokuwa na mimba ni kilogramu 9 hadi 12 kufikia wakati wa
kujifungua. Hata hivyo, wasichana au wanawake ambao hawakuwa wakila chakula cha
kutosha wanapaswa kuongeza kati ya kilogramu 12 hadi 15, na wale
wanene wanapaswa kuongeza kilogramu 7 hadi 9 tu.
MADOKEZO YA KUWASAIDIA WANAWAKE WAJAWAZITO
● Kila siku mwanamke mjamzito anahitaji kula matunda, mboga (hasa zilizo
na majani ya rangi nzito ya kijani, na zenye rangi ya machungwa, au nyekundu),
maharagwe mbalimbali (kutia ndani soya, dengu, na njegere), nafaka (kutia ndani
ngano, mahindi na shayiri - hasa zile ambazo hazijatolewa maganda au zilizotiwa
vitu vingine), chakula kinachotokana na wanyama (samaki, nyama ya kuku, nyama
ya ng’ombe, mayai, jibini, na maziwa, hasa yale ambayo yametolewa mafuta).
Mafuta, sukari na chumvi vinapaswa kutumiwa kwa kiasi. Kunywa maji mengi. Epuka
vinywaji vyenye kafeini, na vyakula vilivyotiwa dawa za kuhifadhi na kemikali
nyinginezo (kama za kutia rangi na ladha). Wanga, udongo wa mfinyanzi, na vitu
vingine visivyoliwa vyaweza kusababisha utapiamlo na kumtia sumu.
No comments:
Post a Comment