JITAHIDI KUZUIA MALERIA WAKATI WA UJAUZITO
Tatizo la
Malaria wakati wa ujauzito na katika watoto linaendelea kuwepo nchini Tanzania
na kote barani Afrika. Ugonjwa huu umesabababisha vifo vingi, hasa kwa
wanawake wajawazito na watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.
Malaria inaua zaidi ya watu milioni moja duniani kila mwaka, wengi wao wakiwa wanaishi Afrika, Zaidi ya vifo milioni tatu vya malaria huripotiwa katika vituo vya afya duniani kila mwaka. Hii ni mara tano ya maambukizi ya kifua kikuu, UKIMWI, surua na ukoma kwa pamoja. Malaria husababisha kifo kimoja kwa kila vifo vinne vya utotoni barani Afrika. Ugonjwa huu huua mtoto wa Kiafrika kila sekunde 30. Wale wanaonusurika kwa maradhi makali ya malaria huweza kuwa na ulemavu mkuu wa kimwili na kiakili.
Ni jambo la kusitikisha kuwa wanawake wana uwezekano mara nne wa kuugua na mara mbili wa kufariki kutokana na malaria endapo ni wajawazito. Nchini Tanzania, asilimia ishirini ya vifo vya wakati wa ujauzito vinatokana na malaria. Wanawake wajawazito na watoto wanaougua malaria huchukua asilimia kubwa ya vitanda hospitalini.

Wataalam
wa kiafya hupendekeza mambo kadhaa kuzuia usambazaji wa malaria.
Pendekezo mojawapo ni kutumia nyavu za vitandani zilizotibiwa kwa dawa ya mbu
manyumbani. Pendekezo lingine ni kuhakikisha boma na maeneo ya karibu nayo
yamepuliziwa dawa. Wanawake wanaoishi katika maeneo yenye malaria
wanapaswa kunywa madawa ya kuzuia malaria kila mara wanapokuwa wajawazito ili
kujikinga wenyewe na pia mtoto aliye tumboni.
No comments:
Post a Comment