SABABU
INAYOWAFANYA WANAWAKE NA WANAUME WENGI KUTOTAKA
KUOA/
KUOLEWA.
Katika
maisha ya vijana wengi wa sasa, tumekuwa kukishuhudia vitendo vingi vya ukatili
kwa wanandoa kiasi ambacho tumepoteza imani sana katika kufikia maamuzi ya
kuoa/ kuolewa.
Kwa
muhtasari tuu, ningependa tuchambue sababu mbali mbali ambazo kiukweli zimekuwa
kiongozi katika kuhakikisha thamani ya kuoa/ kuolewa inashuka au kupotea
kabisa. Na kwa kila kijana ambaye anapenda kubadilika na kujifunza atapata kitu
kipya katika makala hii na hivyo kufunguka kwa namna moja au nyingine katika
swala hili gumu ambalo ndani ya miaka michache ijayo litakuwa janga la kitaifa.
-
Kuingia katika mahusiano ya kimapenzi
kabla ya wakati, hii tukimaanisha katika umri mdogo.
-
Kushuhudia ukatili wa wazi wazi katika
familia uliyoishi au jamii inayokuzunguka ndani na nje ya familia yako.
-
Kupata habari za kukatisha tamaa kutoka
kwa wakubwa zako ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakikushuhudia
kushuka kwa thamani ya kuoa/ kuolewa.
-
Mfumo mbovu wa maisha unayoishi kijana,
kwa kuamini kuwa vigezo na tabia unazohitaji kwa mke/ mume unayemtaka
havijaonekana/ kukupendeza, hivyo unajikuta ukichagua sana.
-
Mara nyingine ni maudhi na kuumizwa
nafsi kutoka kwa mpenzi aliekuacha/kumuacha bila sababu za msingi n.k
Kiukweli
vijana wengi tuna mitazamo mbali mbali kulingana na uchaguzi sahihi juu ya nani
anastahili/kufaa kuwa mwenzi wa maisha yangu, lakini tunakosea sana hasa
inapokuja katika maamuzi,.
Nimeshuhudia
vijana wengi wakipoteza muda katika kuchagua na kuandika vigezo vyao ambavyo
wanahisi ndio key point ya kupata mwenzi, bila kusahau/ kuangalia upande
mwingine wa shilingi, kwamba ‘ Mimi ninavigezo gani kulingana na hivi?’
Jiulize
swali hili kijana unayesoma makala hii, wewe ni PERFECT?
Hivyo
cha msingi hapa ni wewe kujitambua, kuangalia njia zako zipoje na sasa uingie
katika swala la imani na kumuomba Mungu akupe mtu sahihi, ama sivyo utakuwa
ukiwaona wanaume/wanawake wote ni wabaya/si waaminifu katika ndoa, na kubaki
mpweke kwa maisha yako yote.
Jifunze
kusamehe na kusahau, kisha fanya mambo yako kwa mpangilio utaona faaida zake.
Usife
moyo tuzidi kuwa pamoja na tutafundishana na kusaidiana kila wakati,
Imeandaliwa na Diana D. Shirima
Founder - Wanawake Mashujaa Tanzania
No comments:
Post a Comment