KUOA AU KUOLEWA
Maamuzi ya kuoa au kuolewa, si maamuzi madogo, ni moja ya maamuzi makubwa ambayo vijana wengi wa kike na wa kiume wana kutana nayo kila siku. Sasa katika kufanya maamuzi haya ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya vijana mpaka wafike mahali pa kumpata kijana au binti wa kusema huyu ndiye haswa wa kuoana nae , basi ujue tayari wengi wanakuwa walishakosea mara nyingi mpaka kufikia hapo. Wapo ambao wakikosea husema, yule wa kwanza hakuwa chaguo langu, au haukua mpango wa Mungu mwenyewe bali malaika, au utasikia mwingine akisema Mimi sina uhakika sana na wewe kuwa mwenzi wa kudumu.

Je hivi kweli hayo ndiyo yalivyo au
ni ujanja ujanja tu wa vijana tena hasa wa kiume ndio wenye kauli kama hizi.
Lengo la makala hii kwako kijana mwenzangu ni kutaka kukueleza sababu kadhaa
ambazo hupelekea vijana wengi kufanya makosa katika kutafuta mwenzi wa maisha.
vijana Wengi wanakuwa tayari
wameshafanya maamuzi yao wenyewe.
Vijana wengi huwa wanaomba Mungu awape mtu sahihi wa kuishi naye katika maisha yao na wakati huo huo tayari kwenye nafsi yake anakuwa na mtu ambaye ndiye chaguo lake wakuishi Naye kwa sababu hiyo ina kuwa ni vigumu kwao kumpata mtu wa mapenzi ya Mungu na pia ina muwia kazi Mungu kukuonyesha mke au mme wa kusudi lake kwani tayari umeshafanya maamuzi ndani yake, je Mungu afanye nini kama sio kunyamaza.

Sababu zinginezo
Hapa nitaelezea mambo mawili kwa wakati mmoja, la kwanza ni hili kuna vijana huenda wao wenyewe au ndugu zake, wazazi wake walishawahi kumtoa huyo mtoto kama sadaka kwa mapepo kwa sababu ya mila zao au pia alipatikana kwa njia za kipepo. Siri moja ni hii kuna baadhi ya mapepo huwa hayapendi kushare sex na mtu mwingine, hivyo ni lazima yalete kila namna ya upinzani ili mtu asiolewe na wala kuoa. Na mwingine hata kama hakutolewa kama sadaka lakini huenda pepo wameshawahi kufanya mapenzi na huyo mtu na kama yatampenda basi ujue hayatakubali aolewe au kuoa, hivyo yatamletea kila namna ya upinzani katika kuolewa au kuoa kwake. Mengine hufika mahali hata pa kumwachia kijana wa watu harufu mbaya ili mwingine asimpende.

Maneno ya kujitamkia mwenyewe
Kuna baadhi na hasa hapa ni akina dada kwa sababu mbalimbali kama vile kubakwa, kujeruhiwa katika nafsi kwa sababu ya kuachwa na mchumba wake hufikia mahali wakasema mimi sitaki tena kuolewa. Sasa inapofika muda umepita na wanataka tena kuolewa wananaza kuomba Mungu awape mume, wakati huo wamesahau kwamba walishatamka kwamba hawataki tena kuolewa. Nisikilize ukisema hutaki kuolewa au kuoa tena, maana yake unaifunga nafsi yako hapo kwamba hutaoa au kuolewa, na Biblia inasema mtu atashiba matunda ya kinywa chake. Na wakati huo shetani ni mwepesi kufuatilia maneno ambayo ni ya athari kwako. Sasa bila kuondoa hayo maneno kwanza katika nafsi yako na kisha kumuomba Mungu akusaidie katika uamuzi sahihi itakupa mud asana kufikia lengo la kuoa au kuolewa.
Dhambi/ Maswala ya kiimani
Sikiliza Biblia inasema afichaye dhambi zake hatafanikiwa, (Mithali 28:13a). Kuna baadhi ya vijana huwa wanakuwa awali kuna baadhi ya dhambi wamezifanya na hawajazitubia, na bado wana taka mtu awaoe au wa kumwoa. Biblia iko very clear kama kuna dhambi umeficha hutafanikiwa, sasa inategemeana, lakini pia inahusiana sana na kutofanikiwa kwako pia kumpata hata mwenzi tu. Nikupe mfano mara nyingi watu wanatoa mimba, au watoto wanaozaa, nao pia kupata mume au mke huwa inakuwa kazi kweli kweli.
Kutokuenenda kwa Roho.
Paulo anasema, “Basi nasema enendeni kwa roho wala hamtatimiza kamwe tama za mwili” (Wagalatia 5: 16). Kuenenda wa Roho maana yake ni kuongozwa na Roho Mtakatifu, hii ni pamoja na zoezi zima la kutafuta mke au mume. Sasa kwa sababu wewe unaenda kwa mwili, mara eti nataka mtoto portable, mguu wa chupa, mweupeee, nk. Hivyo vitu unavyotaka wewe kuna wengine pia wanataka hivyohivyo na matokeo yake mnaanza kugombaniana msichana au mvulana kwa sababu tamaa za miili yetu zinawaongoza huko.
Kuwa na vigezo binafsi.
Vijana wengi sana katika suala zima la kupata mke ua mume, ukweli wengi wao wana vigezo vingi sana ambavyo kila mmoja angependa huyo mchumba wake awe navyo. Utasikia lazima awe wa kabila ya kwangu, awe portable, mweupee, mrefu ndio mzuri, ajue kutabasamu na kisha awe ana ulamba. Sawa mi sikatai hivyo vigezo, lakini nikuulize swali Je! Unayajua mawazo ya Mungu kuhusu wewe kwa habari ya mkeo au mumeo? Je kibiblia na kijamii hivyo vigezo vyako vinakubalika/ na je mke/mume mtu huchagua mwenyewe au hupewa na Bwana, Najua utaniambia mimi nitaomba Mungu anipe mke/mume mwenye sifa hizo. Ok. Ukiniambia hivyo na mimi nitakuambia kumuomba Mungu kwa muundo huo ni nzuri kabisa, wala sio dhambi lakini kumbuka maandalio ya moyo ni ya mwanadamu lakini jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana. Na hapo ndipo patamu, wengi huwa wanaomba kwa vigezo vyao, na mara nyingi Mungu anapojibu inakuwa tofauti na vigezo vyao, na hapo wengine wanakataa hata chaguo la Bwana wanabakia kuteseka. Jua kwamba wewe unapoweka vigezo vya mwenzi wako na Mungu naye ana vigezo vya aina ya mwenzi anayekufaa.

Kufanya maamuzi kabla ya wakati.
Biblia inasema katika Mhubiri 3:1 “kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu”.Hili ni jambo la kawaida, hata wakati wa uchaguzi kura mtu harusiwi kupiga kama hajafikisha miaka kumi na nane kwa nchi nyingi. Vivyo hivyo hata suala la kutafuta mke au mume lina wakati wake maalumu. Ukitaka kulifanya nje ya kipindi ambacho Mungu amekipanga kwa ajili yako utateseka hadi uchoke. Kumbuka kila mtu ana muda wake, hivyo basi hakuna muda maalumu wa kila mtu kuanza kutafuta mke au mume, bali kila mtu ana muda wake na mara tu unapowadia Mungu humjulisha mtu wake.
Nisikilize ukiulekeza moyo wako upate kujua haya nisemayo na ukajizuia kufanya makosa kama haya, basi nataka nikuhakikishe suala la kupata mke au mume wa kutoka kwa Mungu litakuwa ni jepesi sana,ni sawa sawa na kuombea chakula na ukishafumbua macho ukaanza kula moja kwa moja ukiwa na uhakika kimeponywa na kubarikiwa. Kwa ushahuri zaidi endelea kufuatilia makala hizi na kupenda kujifunza zaidi, bila kuacha kumuomba Mungu.
Imeandaliwa na;
DIANA D. SHIRIMA
Founder - Wanawake Mashujaa Tanzania
No comments:
Post a Comment