Napenda kutumia nafasi hii kuzungumza na kijana mwenzangu ambaye anasoma/ kujifunza kupitia makala hii, kuna mambo mawili au matatu ambayo ningetamani tushirikishane siku hii ya leo, ambayo naamini kwa namna moja ama nyingine yanaweza kubadili mtazamo wako juu ya haya tutakayojadili.
MAHUSIANO YA KIMAPENZI
Mpendwa wangu, napenda nifahamu unalichukuliaje neno hili 'Mahusiano ya kimapenzi' Je? lina uzito wowote au ni neno la kawaida? Na kama lina maana yoyote kwako naomba usisite kunitumia ujumbe wa email katika email hii dianashirima47@gmail.com ili nifahamu jibu lako, na kama kuna swali lolote la binafsi usisite niulize mitakujibu.
1. Katika safari yako yako ya ujana ni changamoto zipi umekutana nazo katika swala zima la mahusiano ya kimapenzi
2. Ulipoanza safari hii ni nini kilisababisha uingie katika safari hii
3. Ni faida gani umeipata/ hasara zipi umepata baada ya kuingia katika safari hii
4. Ushauri wako ni nini kwa vijana walio nyuma yako ambao hawajaingia katika safari hii ya mahusiano ya kimapenzi.
- Hayo ni baadhi ya maswali ambayo nimekuwa nikiwauliza baadhi ya vijana niliobahatika kukutana nao na kuongea nao, natamani kupata majibu yako pia wewe unaesoma makala hii.
Karibu sana tujifunze pamoja, nitaendelea na makala hii mara tu nitakapopokea email zenu na kuzisoma kisha nitarudi na majibu na somo letu lililobakia.
Imeandaliwa
Diana D. Shirima - Mwanaharakati. dianashirima47@gmail.com
No comments:
Post a Comment